KIUNGO tegemeo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amesema kwamba wachezaji wa Azam FC wote wana wazo moja kwa sasa, kupigana kwa uwezo wao wao wote kuhakikisha wanatimiza ndoto za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na tovuti ya klabu baada ya mazoezi ya jana, fundi hiyo wa mpira alisema kwamba wachezaji wa Azam wamekuwa wakihamasishana ndani nan je ya Uwanja juu ya kuhakikisha dhamira hiyo inatimia.

“Kuna ugumu, tunajua. Sote tunajua, lakini hiyo ndiyo dhamira yetu, akili yetu kwa sasa haifikirii chochote zaidi ya ubingwa wa Ligi Kuu, maana yake tupo kwenye mapambano kuhakikisha tunashinda mechi zote zilizobaki,”alisema Sure Boy.
Azam itashuka tena dimbani Aprili 9, kumenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, mchezo ambao awali ilikuwa ufanyike Aprili 6, mwaka huu, lakini ukasogezwa mbele kwa sababu timu hiyo ina wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Ngorongoro Heroes ipo Nairobi tangu jana, kwa ajili ya mechi ya kuwania kucheza Fainali za Vijana Afrika, itakayochezwa Jumapili ya Aprili 6 mwaka huu Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini Nairobi na Azam ina wachezaji zaidi ya watano kwenye kikosi hicho.
Hao ni Aishi Manula, Bryson Raphael, Gardiel Michael, Kevin Friday, Mudathir Yahya, Farid Mussa na Hamad Juma. Wachezaji waliobaki wa Azam FC wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Azam FC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Yanga SC yenye pointi 46 za mechi 22 na Mbeya City yenye pointi 45 za mechi 23.