SHOMARI Kapombe amejiunga na klabu ya Azam FC kufanya mazoezi ili kujiweka fiti kwa wakati huu ambao hana timu baada ya kugoma kurejea klabu yake ya Daraja la Nne Ufaransa, AS Cannes.
Akizungumza na tovuti ya klabu, Kapombe amesema ameamua kuja kufanya Azam FC kwa sababu kwanza ni jirani na eneo analoishi na pia wana vifaa vyote vya vya mazoezi vitakavyosaidia kumuweka fiti.
Hata hivyo, Kapombe hakutaka kuzama ndani juu ya mustakabali wake wa baadaye, akisema; “Nimekuja Azam kufanya mazoezi kujiweka fiti tu, basi,”alisema.

Leave a comment