Kipre Tchetche jana alifunga magoli mawili na kutengeneza mengine mawili katika ushindi wa 4-0 iliyoupata Azam FC dhidi ya Coastal Union na kuifanya ijitanue kileleni mwa msimamo wa ligi.

Kipre alifunga goli la kwanza na la pili kwa klabu yake katika kipindi cha kwanza na kuifanya Azam FC iende mapunziko ikiwa kifua mbele kwa magoli hayo mawili.

Goli la kwanza la Kipre Tchetche lilitokana na juhudi kati yake na kaka yake Kipre Bolou ambao waligongeana vema na kipre kumzunguka mlinzi wa Coasta Union Juma Said Nyosso na kufunga kiufundi.

Beki wa kushoto kinda Gardiel Michale alipiga krosi maridhawa ambayo ilimaliziwa na kipre tchetche kuifanya Azam FC iwe mbele kwa magoli mawili.

Goli la tatu lilifungwa na nahodha John Bocco ambaye alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na kipre Tchetche kabla ya kipre Tchetche tena kufanya kazi nzuri ya kuwatambuka mabeki wa Coastal Union na kupiga krosi iliyomaliziwa na Kevin Friday na kuifanya Azam FC itoke na ushind wa 4-0

Kwingineko kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro kiporo cha Yanga kilichacha baada ya kwenda sare ya 0-0 na Mtibwa huku kule Kaitaba wenyeji Kagera Sugar waliwazima Tanzania Prisons baada ya kuwatungua 2-1