AZAM FC leo itashuka kwenye uwanja wake wa nyumbani kucheza mchezo wa kiporo kati yake na Ashanti United

Mechi itazikutanisha timu za Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 37 dhidi ya Ashanti United iliyoko nafasi ya 12 kwa pointi zake 14.

Ashanti United ndiyo timu pekee iliyofanikiwa kupata sare chamazi katika raundi ya kwanza na leo itajaribu kurejea rekodi yake kwa angalau kuizuia Azam FC kama ilivyofanya Tanzania Prisons wikiendi iliyopita

Kikosi cha Azam FC leo kitawakosa baadhi ya nyota wake kutokana na kuwa na kadi au kuwa majeruhi

Wachezaji ambao watakosekana leo ni Salum Abubakar (Majeruhi) John Bocco na Kipre Tchetche (kadi)

Azam FC huenda ikawatumia baadhi ya chipukizi wake toka kwenye academy ili kuziba pengo hilo