KOMBE la Mapinduzi limezidi kunoga baada ya timu bora nne kutinga hatua ya nusu fainali ambaya itachezwa kesho.

Azam FC ilikuwa timu ya kwanza kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya mchana wa leo kuilaza mabao 2-0 Cloves Stars Uwanja wa Gombani Pemba.

Mabao yaliyoipeleka Azam Nusu Fainali yalifungwa na mabeki Aggrey Morris dakika ya 68 na Waziri Salum dakika ya 85 baada ya kupokea pasi ya Ibrahim Mwaipopo

Aggrey alifunga bao lake kwa guu lake la kulia baada ya kuuwahi mpira uliorudi kufuatia yeye mwenyewe kuunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Malika Ndeule.

Waziri naye alifunga bao lake baada ya kupokea pasi maridadi ya ‘kiungo aliyehamishwa namba toka kiungo ukabaji hadi ushambuliaji wa kweli’ Ibrahim Mwaipopo akiwa ndani ya sita na kumchambua vizuri kipa wa Karafuu.

Azam sasa itakwaana na KCC ya Uganda mechi huku Simba itaikabili URA katika mechi itakayochezwa usiku

Baada ya kurejea toka pemba kucheza mechi jana hiyohiyo, kocha wa Azama FC Marius Omog alisema mechi sita alizocheza mpaka sasa zimemsaidia kuwajua wachezaji wake ambapo sasa ameshapata wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza na nafasi mbili ndizo ambazo anaendelea kuzifanyia kazi

Kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Malika Ndeule/Saleh Abdallah, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Farid Mussa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Umony/Muamad Kone, Kipre Tchetche/Seif Abdallah na Khamis Mcha ‘Vialli’/Ibrahim Mwaipopo.