Azam FC leo itashuka kwenye uwanja wa Amaan saa kumi jioni kukwaana na timu ya Combine ya Unguja katika mchezo wa kwanza kwa mabingwa watetezi wa Mapinduzi Cup

Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza kwa kocha Marius Joseph Omog ambaye amejiunga na Azam FC mwezi mmoja uliopita akitokea kwa mabingwa wa Congo Republic AC Leopards

Kocha Marius Omog tayari ameona matatizo kwenye timu ambapo anasema washambuliaji wengi wa pembeni (wingers) wanacheza kama washambuliaji wa kati na ukichunguza utagundua kuwa ni kweli washambuliaji wa pembeni wa Azam FC (Kipre Tchetche, Joseph Kimwaga na Brian Omony) kiasili ni washambuliaji wa kati hivyo kocha anaposema wanacheza kama washambuliaji wa kati ni rahisi kumuelewa ukifuatilia historia za wachezaji hawa.

Licha ya hilo, kocha amefurahishwa sana na viwango vya wachezaji wote kuwa ni vya hali ya juu sana… na ana matumaini kuwa akiweza kurekebisha kasoro ndogo za mawinga timu itakuwa kwenye uwezo wa kupambana na timu yoyote Afrika.

Mfumo mpya wa kocha Omog ni kukaba kwa bidii na kumiliki mpira…. Kocha anataka timu idhibiti mpira, anasema ukidhibiti mpira unakuwa umedhibiti mchezo.

Nahodha John Bocco atakosa mchezo huo kutokana na sababu za kiafya
Baadaye tutawaletea kikosi kitakachoanza leo kwenye Facebook Page ya klabu