Mabingwa watetezi wa Kombe la Uhai Azam Academy' imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ya vijana walio chini ya miaka 20 ya vilabu vya ligi kuu Tanzania baada ya kuifunga Tanzania Prisons 2-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

 

Matokeo hayo ya robo fainali yanaivusha Azam Academy hadi hatua hiyo ambapo watacheza dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa nusu fainali utakaochezwa siku ya Ijumaa katika uwanja huo huo.

 

Katika mchezo wa jana jioni Azam Academy walikuwa wa kwanza kupata goli katika dk ya 13 kupitia kwa Mange Chagula na kupeleka timu mapumziko Azam Academy wakiwa mbele 1-0 dhidi ya Prisons.

 

Kipindi cha pili Azam Academy walipata bao la pili kupitia kwa Erick Haule na kuifanya timu hiyo ikiongoza 2-0 Prisons, Prisons walipata bao dk 83 lililofungwa na Awadh Athuman na kumaliza mchezo Azam Academy 2-1 Prisons.

 

Prisons imeungana na JKT Oljoro kuyaaga mashindano hayo JKT Oljoro ilifungwa 1-0 na Coastal Union