Mashindano ya Uhai Cup 2013  yameingia kwenye hatua ya Robo Fainali ambapo mechi za robo fainali zitaanza kesho

Azam Academy ambayo ilifaidika na ushindi wa Ruvu JKT dhidi ya Yanga na kutinga robo fainali ikiiacha Mbeya City ambayo kabla ya matokeo hayo ilikuwa kama imefuzu itakwaana na Tanzania Prisons hapo jioni

Simba moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kufanya vema kwenye mashindano haya itakwaana na Mtibwa Sugar huku wapinzani wao wa jadi Yanga wakikwaana na timu bora na ngumu kwenye mashindano haya mwaka huu ya Ashanti

Wagosi wa ndima, waja leo waondoka leo Coastal Union wao watakwaana na maafande wa JKT Oljoro na kuhitimisha robo fainali hizi hapo kesho kutwa

 

Kwa mujibu wa Ratiba Mshindi kati ya Azam Academy na Prisons atakwaana na Mshindi kati ya JKT Oljoro na Coastal Union huku mshindi kati ya Simba na Mtibwa akikwaana na mshindi kati ya Ashanti United na Yanga