Joseph Kimwaga jana alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa mara nyingine tena akiwaangusha Ramadhani Singano wa Simba na Juma Luizio wa Mtibwa

Kimwaga ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana na ambaye majuzi kocha mkuu wa timu ya taifa Kim Paulsen amemjumuisha kwenye kikosi chake cha wakubwa alikuwepo kwenye hafla hiyo akisindikizwa na nahodha wake Mgaya Abdul na kupokea tuzo yake yeye mwenyewe kama anavyoonekana pichani