Kipre Tchetche jana alitwaa tuzo mbili za Mwanaspoti kutokana na kiwango alichokionesha msimu uliopita.

Kipre Tchetche alishinda tuzo ya ufungaji bora wa ligi kuu Vodacom akiwa na magoli 17 kabla ya baadaye kushinda tena tuzo ya kuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 11 bora wa VPL.

Kikosi hicho kinaundwa na Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, David Mwantika, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, Haruna Niyonzima, Themi Felix, Mbwana Samatta na Kipre Tchetche.

Mchezaji mwingine wa Azam FC aliyeshinda tuzo ni David Mwantika ambaye kwa bahati mbaya hakuwepo ukumbini na zawadi yake kuchukuliwa na mwakilishi wake. David alishinda tuzo ya kuwa Sentahafu Bora wa msimu uliopita.

Joseph Kimwaga jana alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa mara nyingine tena akiwaangusha Ramadhani Singano wa Simba na Juma Luizio wa Mtibwa

Kimwaga ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana na ambaye majuzi kocha mkuu wa timu ya taifa Kim Paulsen amemjumuisha kwenye kikosi chake cha wakubwa alikuwepo kwenye hafla hiyo akisindikizwa na nahodha wake Mgaya Abdul na kupokea tuzo yake yeye mwenyewe kama anavyoonekana pichani.