AZAM TV leo itakuonesha mchezo kati ya Azam FC vs Mbeya City Live toka Chamazi kupitia Chanel 10 na TBC2 kuanzia saa kumi jioni hii

Huu ni Mchezo ambao umewafanya wadau wa soka wasahau kuwa kuna mechi nyingine viwanja vingine… kila mtu anazungumzia Azam FC vs Mbeya City… ikiwa vilabu vingi zaidi vitajiimalisha kama ilivyo Mbeya City basi soka letu litakua,

Azam FC inafurahia ushindani ulioletwa na Mbeya City na ingependa kuona ushindani huu unaimarishwa na kupewa sapoti na wadau wote (wa Mbeya na Wenye asili ya Mbeya Nje ya Mbeya) maana Azam FC iliondoa top two na kuleta top three sasa Mbeya City Imeleta top Four… Tunatarajia kandanda safi na ya ushindani leo… Timu bora uwanjani Itashinda….

Kikosi cha Azam FC kiko vizuri na kimejipanga kuhakikisha kuwa kinaondoka na pointi tatu

Jeshi la Polisi pia limetuhakikishia kuwa kutakuwa na ulinzi wa kutosha kuhakikisha kuwa wachezaji, waamuzi na watazamaji wanashiriki kwenye mchezo huu bila bughdha

Karibuni Chamazi Stadim na kama upo mbali Tazama Chanel 10 na TBC2 kuanzia saa kumi kamili jioni