Azam FC leo itatua kwenye dimba lake la Chamazi kukwana na timu ngumu na bora msimu huu ya Ruvu Shooting Stars

Azam FC yenye pointi 23 pasi na kupoteza mchezo wowote itajaribu kuendeleza rekodi yake ya kushinda mechezo yake mfululizo ambapo hadi sasa imeshinda michezo minne mfululizo na kuwa nyuma ya Mbeya City Council iliyoshinda michezo mitano mfululizo hadi sasa.

 Timu hizi mbili za Azam FC na Mbeya City Council ndizo timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo hata mmoja hadi hivi sasa na zitakutana alhamisi Novemba 7 kwenye uwanja wa Chamazi.

Akizungumza na tuvuti hii, Meneja wa Azam FC Jemedary Said amesema wao kama Azam FC wamedhamiria kushinda michezo yake hii miwili ya mwisho ili kuweza kuongoza ligi baada ya raundi ya kwanza kuisha.

Wachezaji wa Azam FC wakiongoza na manahodha wao John Bocco, Jabir Aziz na Himid Mao wameahidi pia kupigana kufa na kupona kuhakikisha timu inaondoka na pointi zilizosalia kwenye raundi hii ya kwanza.