AZAM FC imekaa kileleni mwa Ligi Kuu, baada ya jana kushinda bao 1-0 dhidi ya JKT Oljoro na kufikisha pointi 20 katika mechi kali iliyochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Bao hilo pekee lilifungwa na Hamis Mcha dakika ya 79, kutokana na mpira wa adhabu iliyokwenda moja kwa moja.

Kutoka Turiani, Morogoro, Mtibwa Sugar imepanda hadi nafasi ya nne ikifikisha pointi 16 baada ya kuichapa Mgambo Shooting mabao 4-1.

Naye Kenneth Ngelesi anaripoti kutoka Uwanja wa Sokoine Mbeya kuwa Mbeya City, nayo imefikisha pointi 20, hivyo kukamata nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani.

Bao la vijana hao wa Kocha Juma Mwambusi, lilipachikwa wavuni na Jeremiah John katika dakika ya 36, baada ya kufanya shambulizi kali langoni mwa JKT Ruvu.

Katika Uwanja wa Azam Complex, Ashanti United imetoka sare ya 2-2 na Ruvu Shooting.
Source: Tanzania Daima