Azam FC inashuka dimbani leo kukwaana na Yanga SC katika mechi ya Ngao ya Hisani itakayochezwa uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam

 

Gazeti la Nipashe limeandika kuwa Azam FC ikiifunga Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Bara leo kama rekodi za mapambano baina ya timu hizo tangu kuanza kwa muongo huu itaendelea.Tangu mwaka 2010, mabingwa wa ligi kuu ya Bara Yanga na washindi wa pili Azam zimekuwa zikifungana msimu mzima mfululizo kwa zamu katika mechi za mashindano.


Na kwa sababu historia inaonyesha zamu ya Yanga inaweza kuwa imeisha, timu ya wauza vyakula huenda ikatwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza katika historia yake fupi kisoka.Lakini hiyo ni historia tuu, kwenye mchezo wa soka huwezi tegemea historia, Yanga ni Mabingwa wa Tanzania kwa sasa na wana kikosi imara sana na kocha wao ni bora hivyo wanaweza kupata matokeo mazuri endapo bahati itakuwa yao.

Mtandao wa Azam FC unaitakia kila la kheri klabu ya Azam FC kwenye mechi ya leo