Kikosi cha Azam Academy kilichoitoa Coastal Union kwa penati leo na kutinga fainali za Rolling Stone, katika mechi tano ilizokwisha cheza Azam Academy imefunga magoli 11, Haijafungwa goli hata moja na haijapoteza mchezo hata mmoja. imeingia Fainali na sasa itacheza na Eagle Rangers ambayo nayo imeifunga JKT Oljoro 2-0. 

Eagle Rangers ilikuwa kundi moja na Azam Academy na katika mchezo wa ufunguzi ilifungwa 3-0

Kabla ya penati mechi timu hizo zilimaliza muda wa kawaida zikiwa hazijafungana (0-0). 

Mikwaju ya penati ya Azam Academy ilifungwa na Abdul Mgaya, Ismail Adam Gambo, Kelvin Friday, Adam Shoba na Abdalah Shirazi

Azam Academy itakutana na Eagle ya Tanga katika mchezo wa fainali itakayochezwa siku ya Jumanne, timu hizo zinakutana kwa mara ya pili baada ya kucheza hatua ya makundi ambapo Azam Academy waliifunga Eagle 3-0.

Pongezi kwa wachezaji wa Azam Academy, tunawatakia kila la kheri!!!!!!!!