Azam Academy jana ilicheza na timu ya Ligi kuu ya Ashanti United kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume Ilala na kushinda kwa bao moja bila goli likifungwa na Mshambuliaji wa pembeni toka shinyanga Mange

Vijana wa Azam Academy wanaonolewa na kocha Vivek Nagul akisaidiwa na Iddi Cheche chini ya meneja Philip Alando walicheza kandanda safi na kuwapoteza kabisa vijana wa Ashani United wanaocheza ligi kuu Tanzania.

Mechi hii ya kirafiki ni ya tatu ndani ya siku nne ambapo siku ya jumatano Azam Academy ilishuka kwenye uwanja wake wa nyumbani na kukwaana na timu ya Transit Camp inayoshiriki ligi daraja la kwanza na kuiangushia kipigo cha 3-1, katika mchezo huo ambao uliacha gumzo kutokana na Azam Academy kutawala mchezo huo wakipiga pasi wanavyotaka.

Baada ya mechi hiyo viongozi wa Transit Camp walikwenda kwa uongozi wa Azam FC na kuwapongeza na kusema kama timu hii ingekuwa inashiriki ligi daraja la kwanza hakika ingeweza kupanda ligi kuu bila matatizo yoyote.

Wachezaji wanaotia fora kwenye kikosi hicho ni Kaijage, Rey, Dismas, Kevin Friday, Mkomola, Mgaya, Mange, Adam Juma, Jamir Brison na Adam Gambo.

Jumamosi Asubuhi licha ya kucheza vizuri na kutawala sehemu kubwa ya mchezo lakini walijikuta wakipokea kipigo cha goli moja bila bao likifungwa na Brian Umony ambaye alitumia vizuri mchezo wa mtego wa counter attack

Kutokana na timu kuwa kwenye maandalizi ya Mashindano ya Rolling Stone, hakutakuwa na majaribio ya kawaida ya kila tarehe mosi mwezi huu wa saba. majaribio yataendelea kama kawaida Tarehe 1/8/2013… Imetolewa na benchi la ufundi la Azam Academy