Wachezaji wote wanne waliosimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi yao wameripoti kambini tayari kuikabili Simba SC siku ya jumapili

Pichani Juu Aggrey Morris na Erasto Nyoni wakifuatilia mchezo kati ya Azam FC na African Lyon, Picha kwa hisani ya Blogu ya Binzubeiry

Kurejea kwa wachezaji hao kunamaliza mgogoro uliokuwepo na kudumu kwa takribani miezi mitano kufuatia shutuma za rushwa ambazo zilipelekwa takukuru kuchunguzwa ili kujua ukweli na uongozi wa Azam FC unaishukuru takukuru kwa kazi nzuri ambapo imegundulika kuwa wachezaji hao hawakuhusika na hivyo kusafishwa na chombo hicho chenye mamlaka ya kuchunguza tuhuma za rushwa.

Wachezaji hao wote wanatarajiwa kuwemo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba SC ikiwa mwalimu ataona inafaa na wapo katika hali nzuri kuweza kucheza.

Mchezo huo wa jumapili ni muhimu sana kwa Azam FC kwani ikishinda itaizidi Simba SC pointi 14 huku simba ikisaliwa na michezo minne na hivyo kumaanisha kuwa Kagera Sugar atabaki kuwa mpinzani pekee wa Azam FC katika kuwania nafasi ya pili.