Goli la mshambuliaji mwenye makeke na kipaji cha hali ya juu Kipre Herman Tchetche jana lilitosha kuifanya Azam FC kuondoka uwanjani na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu shootig katika mchezo mkali uliofanyika kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani

Ushindi huo unaiweka Azam FC karibu kabisa na malengo yake ya kushika moja kati ya nafasi mbili za juu kwani sasa inaizidi Kagera Sugar inayoshika nafasi ya tatu kwa pointi sita huku kagera ikiwa na mchezo mmoja zaidi na ikisaliwa na michezo minne tuu.

Mchezo wa jana ambao ulivunja rekodi ya mashabiki mkoani Pwani ulikuwa mkali na wa kusismua muda wote ambapo wachezaji Luckson Kakolaki, Himid Mao, Jockins Atudo na Waziri Salum walifanya kazi kubwa na nzuri ya kulinda lango lao wakiongozwa na kinda Aishi Salum golini

Azam FC ilipata goli lake baada ya Kipre Tchetche kumchambua kama karanga mlinzi mmoja wa Ruvu Shooting, 

Mchezaji John Bocco alikosa magoli kadhaa huku Salum Abubakar na Kipre Bolou wakifunika eneo la kiungo ingawa walikutana na ushindani mkubwa toka kwa kiungo kinda na nyota kwa sasa nchini Hassan Dilunga

Azam FC imerejea jijini jana hiyo hiyo na leo inakula mapumziko ya sikuku ya Pasaka kabla ya kuanza kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya BYCii hapo jumanne