Timu ya Azam FC kesho itashuka kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kukwaana na Tanzania Prisons katika mfululizo wa ligi kuu ya Vodacom

 

Azam FC yenye pointi 37 itahitaji kushinda katika mchezo wa kesho ili kujiimarisha katika nafasi ya pili na kuweza kuiwakilisha tena nchi kwenye michezo ya Kimataifa ambao hadi sasa ina ushindi wa 100% kwenye mechi za kimataifa baada ya kucheza mechi tatu na kushinda zote

Tanzania Prisons ambayo inapambana kuhakikisha inasalia kwenye ligi kuu itakuja uwanjani kwa nia ya kushinda ikiongozwa na kocha wake mtundu mwenye mbinu nyingi Jumanne Charles

Wachezaji wate wa Azam FC akiwemo Brian Umony wapo katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo isipokuwa David Mwantika anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu kutokana na kupewa kadi nyekundu mchezo uliopita na Haji Nuhu aliye majeruhi

Timu ya Azam FC iliingia kambini jana jumatatu jioni kujiandaa na mchezo huo