Kiungo mwenye mapafu ya mbwa Abdulhalim Humud Gaucho huenda akasafiri kuelekea bondeni Afrika ya Kusini wikiendi hii kufuatia kupata nafasi ya majaribio kwenye timu ya Jomo Cosmos aliyowahi kuchezea watanzania mengine Nteze John na Ally Shah siku za nyuma

Cosmos inayomilikiwa na kocha wa zamani wa Bafana Bafana Jomo Sono imempa nafasi hiyo humudi baada ya kufanyiwa mipango na uongozi wa Azam FCkatika kutekeleza sera yake ya kutengeneza uwanja mkubwa kwa wachezaji wa kitanzania kwenye ligi mbalimbali zinazoendeshwa kisasa.

Cosmos ambao wapo kwenye kampeni ya kurejea PSL watahitaji huduma ya Humud msimu ujao ambao Jomo Sono ameahidi kuwa watakuwa wakicheza PSL