Azam FC inashuka kwenye uwanja wa taifa wa South Sudan kukwaana na askari wa Al Nassir katika mchezo wa marudiano wa CAF Confederations Cup

Mchezo huo ambao utarushwa moja kwa moja na kituo cha Star TV kwa huko nyumbani ambao watashirikiana na South Sudan TV na kuonekana karibu Afrika nzima kupitia ving'amuzi vya DSTV-kwa Star TV na ARAB – SAT kwa upande wa South Sudan TV umevuta hisia za wananchi wengi wa hapa Juba

Azam FC leo inatarajiwa kupangwa kama ifuatavyo

Mwadili Ally, Himid Mao, Wazir Salum, David Mwantika, Jockins Atudo, Kipre Bolou, Humphrey Mieno, Salum Abubakar, John Bocco, Kipre Tchetche na Khamis Mcha Viali

Mungu ibariki Azam FC, Mungu ibariki Tanzania