Timu ya soka ya Azam FC imesafiri leo kuelekea Manungu Turiani mkoani Morogoro kukwaana na Mtibwa Sugar mchezo ambao utafanyika kesho

Azam FC imesafiri na kikosi chake chote cha wachezaji 25 na viongozi nane ambao ni Dr Twalib, Gomes, Kally Ongala, Jemedary Said, Iddi Abubakar, Ibrahim Shikanda na Stewart Hall.

Wachezaji wa kigeni waliokuwa na majukumu katika timu za taifa, Humphrey Ochieng Mieno na Jockins Atudo walirejea jana usiku huku Brian Umony akiwasili hapo mchana jana.

Leo asubuhi kabla ya safari Azam FC ilifanya mazoezi kwenye kambi yake iliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam

Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 30 nyuma ya Yanga yenye pointi 33 na Simba ikishika nafasi ya tatu ikiwa n pointi 27