Golikipa kinda toka Azam Academy ambaye pia huitwa kikosi cha timu ya Taifa Stars Aishi Salum Manula leo alikuwa shujaa langoni baada ya kuzuia michomo ya Sofapaka dakika za mwisho wa mchezo na kufanya matokeo yabakie 1-0 kufuatia Azam FC kupata goli kwa njia ya penati lililofungwa na Gaudence Mwaikimba kipindi cha kwanza

Huu ulikuwa mchezo wa pili kwa Azam FC baada ya kupoteza mchezo wa kwanza 2-1 dhidi ya AFC Leopards

Azam FC ipo nchini Kenya ikiendelea na maandalizi ya ligi kuu Vodacom, sasa imebakisha mchezo mmoja ambapo itakwaana na KCB siku ya jumanne