Azam FC jioni hii inatua kwenye uwanja wa taifa wa Nyayo jijini Nairobi kukwaana na AFC Leopards “IGWE” katika mchi yake ya kwanza ya kirafiki jijini Nairobi kujiandaa na ligi kuu ya Vodacom  na Mashindano ya CAF Confederations Cup

Pichani juu Azam David Mwantika akiwaongoza wachezaji wenzake kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa leo kwenye uwanja wa Nyayo jana jioni

 

FC vs SOFAPAKA kesho Nyayo Stadium

Azam FC inaendelea na maandalizi ya siku saba jijini Nairobi, kesho watacheza mchezo wake wa pili dhidi ya SOFAPAKA ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyayo.

 

Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema mechi itakuwa nzuri kwake kutokana timu hizo kucheza mchezo wa aina inayofanana baada ya kuzifundisha timu hizo.

 

Stewart alisema mechi hiyo muhimu kwake itakuwa na sura tofauti kwa kukutanisha wachezaji waliopata mafunzo kupitia kwake, hivyo mbinu na aina nyingine ya mchezo bado SOFAPAKA wanaitumia.

 

"Nataraji kuona wachezaji wangu wote wakifanya vizuri hasa wa Azam FC, kupambana na timu uliyoifundisha kunakuwa na ugumu, wanaweza kucheza wakifanana kila sehemu hali itakayopunguza idadi ya magoli kwa moja ya timu hizo” alisema Stewart.

 

Alisema wachezaji wake wanaonekana kucheza vizuri kipindi hiki, wamezoea hali ya hewa ya Nairobi hivyo mchezo na SOFAPAKA watakuwa na kila sababu ya kufanya vizuri.

 

Naye Kocha wa SOFAPAKA David Ouma alisema kukutana na Azam FC katika mechi ya kirafiki ilikuwa moja ya mipango yao, wanatarajia kucheza mchezo wa ushindani zaidi na kuwapa nafasi wachezaji wake wapya waliosajiliwa hivi karibuni.

 

“Haya ni maandalizi mazuri kwa timu yangu, tumeanza mazoezi wiki mbili zimepata, kupitia mechi hii tutajua maendeleo ya timu, wachezaji hasa hawa tuliowasajili, pia tutazidi kujenga urafiki mzuri na Azam FC” alisema kocha Ouma.

Azam FC baada ya mchezo huo, siku ya Jumatatu itapumzika kwa kufanya mazoezi, na kumaliza mchezo wake wa tatu siku ya Jumanne dhidi ya K.C.B utakaochezwa kwenye Uwanja waNairobi  City uliopo jijini hapa.

 

Timu hiyo inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania mzunguko wa mwisho wa ligi utakaoanza Jan 26 mwaka huu.

 

 

 

Atudo, Mieno ndani ya Harambee Stars

Wachezaji wa Azam FC, Jockins Atudo na Humphrey Mieno wameitwa kuunda timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Libya utakaochezwa Feb 6 mwaka huu nchini Tunisia.

 

Akizungumza jana na www.azamfc.co.tzkocha mkuu wa Harambee Stars, James Nadwa amesema amewaita wachezaji hao kutokana na mchango wao waliounyesha kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji mwaka jana pamoja na uwezo wakiwa na klabu yao ya Azam FC.

 

“Nimekuwa nikuwafatilia mara kwa mara wanaonekana kuwa na viwango vizuri, wanasaidia timu yao kwangu naona wanastahili kuwa moja ya wachezaji watakaounda timu yangu ili kuongeza nguvu zaidi” alisema kocha Nandwa.

 

Kocha huyo alisema ameita jumla ya wachezaji 24, wachezaji tisa katika yao ni wachezaji wanaocheza soka la kulipwa ambao ni Atudo na Mieno, wengine ni Denis Oliech wa Ufaransa, MacDonald Mariga anayecheza Italia, Arnord Otieno aliyeko Norway, Brian Mandela na David Gateri waliopo Afrika Kusini, Victor Wanyama wa Scotland na Ayub Timbe anayekipiga Belgium

 

Mchezo huo ulioko katika kalenda ya FIFA utachezwa nchini Tunisia kutokana na Libya kuwa na matatizo yanayopelekea mechi kutochezwa kwenye aldhi ya nchi hiyo.

 

Alisema kambi itaanza tarehe 24 kwa wachezaji wa ndani wachezaji wanaotokea nje ya nchi watajiunga kuanzia February 1 timu hiyo inatarajiwa kuelekea nchini Tunisia tarehe tatu kwa maandalizi ya siku mbili kabla ya mechi hiyo.

Baada ya mchezo huo timu itarejea nchini Kenya na kuanza maandalizi mengine ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014, wataocheza dhidi ya timu ya Taifa ya Nigeria.