FAINALI ya Saba katika mashindano nane katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, ikitwaa ubingwa mara tatu na kuteleza mara nne tuu. Hii ndiyo Azam FC

Unaweza kuita majigambo ya mwandishi wa makala hii lakini huu ndiyo ukweli na hakuna lugha nyingine ya kutumia zaidi ya kuiita Fainali ya saba ndani ya miezi 12

Azam FC iliyopanda daraja la juu miaka mitano iliyopita baada ya kusuasua kwa miaka mingi ikijenga uwezo wake sasa imekuwa kamili kwa michuano ya ndani huku ikiendelea kujijenga kwa ajili ya mashindano ya Afrika

January 12, mwaka jana Azam FC ilifika fainali za Mapinduzi Cup kwa mara ya kwanza na kutwa kombe baada ya kuifunga Jamhuri 3-1,

Baada ya hapo Azam FC ilirudi kwenye ligi na kushinda mechi 11 na kupoteza mechi mbili tuu, kwa matokeo hayo Azam FC ilishika nafasi ya pili kwenye ligi na kupata nafasi ya kucheza CECAFA Kagame Cup na CAF Confederations Cup

Miezi mitano baadaye Azam FC ilifika hatua ya fainali ya kombe la ujirani mwema na kucheza na Simba SC uwanja wa Taifa na kufungwa kwa mikwaju ya penati baada ya timu kutoka sare 2-2 katika muda wa kawaida wa dakika 120

Mwezi July 2012, Azam FC ilitinga tena fainali, safari hii ikiwa fainali ya mashindano makubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki, yaani CECAFA baada ya kuzisukuma nje ya mashindani vigogo vya AS Vita ya DRC na Simba SC ya Dar es Salam katika michezo ya robo fainali na nusu fainali. Azam FC ilicheza fainali na Yanga na kufungwa 2-0

Mwezi wa Agosti Azam FC ilicheza mashindano ya Bank ABC Super 8 na kuondolewa na Simba SC kwenye nusu fainali kabla ya kurejea kwenye ligi kuu ambako hadi sasa inashika nafasi ya pili.

Azam FC kupitia kikosi chake cha Under 20 ilicheza fainali yake ya nyingine hii ikiwa ya Uhai Cup na kutwaa kikombe baada ya kuitandika Coastal Union kwa mikwaju ya penati 3-1

Siku hiyo hiyo kaka zao walikuwa wakicheza fainali Congo Charity Cup mjini Kinshasa na kutwaa kikombe baada ya kuifunga Dragons kwa mikwaju ya penati pia baada ya mapokeo ya  sare. Hiyo ilikuwa fainali ya tano na kikombe cha tatu.

 

Leo hii Azam FC inaingia Fainali tena kwa mara ya saba katika mashindano manane tofauti na itacheza na Tusker ya Kenya. Tunaiombea dua timu yetu ishinde na kuongeza vikombe kwenye kabati lake…

 

 

 

 

S.N

Mwezi

Mashindano

Matokeo

1

January 2012

Mapinduzi Cup

Fainali/Ubingwa

2

April 2012

Ligi Kuu

Nafasi ya Pili

3

 June

Urafiki Cup

Fainali

4

July 2012

CECAFA Kagame Cup

Fainali

5

August 2012

Ngao ya Jamii

Nafasi ya pili

6

December 2012

Uhai Cup

Fainali/ Bingwa

7

December 2012

Congo Charity Cup

Fainali/Bingwa

8

January 2013

Mapinduzi Cup

Fainali