Kampuni ya kutengeneza vyakula na vinywaji baridi ya SSB ambayo pia ni wadhamini na wamiliki wa klabu ya Azam FC wameingia kandarasi na kituo cha televisheni cha Star TV kurusha matangazo ya mchezo wa kesho wa fainali ya Mapinduzi Cup

Fainali hiyo ambayo itawakutanisja mapingwa wa Kenya Tusker FC na Mabingwa watetezi wa Mapinduzi Cup Azam FC itachezwa kwenye uwanja wa Amaan usiku wa kesho kuanzia saa mbili na nusu

Katika mchezo wa Kesho, mbali na wachezaji waliopo Ethiopia na timu ya Taifa, pia  Azam FC itawakosa wachezaji wake sita muhimu wanee wakiwa na majeruhi na wawili wakitumikia adhabu baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi ya nusu fainali.

Wachezaji watakaokosekana ni Aishi Manuala (Timu ya Taifa) Waziri Salum (majeruhi) Ibrahim Mwaipopo na Jabir Aziz (Kadi Nyekundu) Abdulhalim Humud na Abdi Kassim (Majeruhi) Salum Abubakar na Hamis Mcha (Timu ya Taifa) John Bocco na Kipre Tchetche (Majeruhi

Katika kuziba mapengo hayo, Azam FC imewapeleka Zanzibar wachezaji wa timu ya vijana ambao ni Reyna Mgungira, Jamir Reuben Mchaulu na Samuel Mkomola

Pichani Juu Wachezaji wa kimataifa wa Azam FC wakifuatilia mpambano kati ya Miembeni na Tusker FC, Kutoka kushoto ni Brian Umony, Katikati ni Kipre Bolou na kulia ni Humphrey Mieno (Picha kwa hisani ya blogu ya BinZubeiry)