Wachezaji wapya wa kimataifa waliosajiliwa hivi karibuni, Brian Umony, Jockins Atudo na Humphrey Mieno, David Mwantika, Seif Abdallah na Uhuru Selemani wameanza vizuri katika kikosi hicho kwa kutoa mchango mkubwa kipindi hiki cha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

 

Kwa nyakati tofauti wachezaji hao wameweza kumudu nafasi zao vizuri hali iliyomuondoa shaka kocha msaidizi wa kikosi hicho Kali Ongala.

 

Kali ameiambia tovuti hii www.azamfc.co.tzkuwa wamepata mchango mkubwa kutoka kwa wachezaji hao, wameonyesha umahiri wao na uwezo wa kwa kipindi kifupi walichojiunga na timu hiyo.

 

“Tunafura wanafanya visuri, yalikuwa matarajio yetu kupata wachezaji mahiri kama wao, wamefanya vizuri kadri muda unavyokwenda, tunaamini wakikaa Chamazi kwa pamoja watatoa mchango wao zaidi ya hapa” alisema Kali.

 

Kali aliongeza kuwa wachezaji hao mbali na kufanya vizuri uwanjani wapo karibu sana na wachezaji wenzao hali inayowapa ukaribu na kujenga timu moja hata wanapokuwa uwanjani.

 

Azam FC wakati wa dirisha dogo la usajili imesajili wachezaji hao watatu wa kimataifa, mshambuliaji Umony kutoka Uganda, kiungo Mieno na beki Atudo wote kutoka Kenya.

 

Mbali na hao wachezaji wa aliotoka nadni ya nchi ni Uhuru Selemani, David Mwantika na Abdalah Seif.