Mabingwa watetezi wa Mapinduzi Cup Azam FC imeanza taratibu michuano baada ya kutoka sare ya 0-0 na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.

 

Katika Mchezo wa leo nahodha wa Azam FC alikuwa ni Himid Mao “pichani juu”, mchezaji chipukizi mwenye umri wa miaka 21 tuu lakini akiwa mmoja kati ya wakongwe kikosini kutokana na kuwa na msimu wanne na Azam FC

 

Azam walipata nafasi nzuri za kufunga kupitia kwa Seif Rashid, Kipre Tchetche, Jockins Atudo na Gaudence Mwaikimba lakini umaliziaji haukuwa mzuri.

 

Coasta Union walitawala kipindi cha kwanza na Azam FC kutawala kipindi cha pili, kwa maana hiyo kwa ujumla mechi ilikuwa 50/50

 

Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Seif Abdallah dk 66. 

Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph Mahundi dk 90. 

 

Picha kwa hisani ya Blogu ya Binzubeiry