Kikosi cha Azam FC kipo katika hatua za mwisho za maandalizi kwa ajili ya kutetea Kombe la Mapinduzi 2013 litakaloanza jumatano ijayo visiwani Zanzibar.

Azam FC itaondoka baada ya Mwaka Mpya 2013 tayari kulitetea kombe hilo walilochukua mwaka huu katika fainali baada ya kuifunga 2-1 timu ya Jamhuri ya kutoka Pemba.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala ameiambia www.azamfc.co.tzkuwa wanajiandaa vizuri kuhakikisha wanarudi na kombe hilo kwa mara ya pili.

Kali amesema katika mashindano hayo watafanya kazi zaidi ya ilivyokuwa nchini Congo walipokuwa wanashiriki Kombe la Hisani kwa kuwa kikosi hicho kinawachezaji mahiri na wanaojua majukumu yao.

“Tumejiandaa na tuko vizuri, timu ina wachezaji wazuri wanaoweza kushindana hivyo sidhani kama tunaweza kulikosa kombe hilo, tunataka tulilete tena klabuni kwetu” amesema Kali.

Amesema kutetea ubingwa huwa ni kazi na kunahitaji maandalizi makubwa, kuzingatia hilo, wamewaandaa wachezaji katika hali zote, kuhakikisha hawapotezi nafasi hiyo muhimu kwao.

 

Ratiba kamili ya Mapinduzi Cup ni

 

 

2013 MAPINDUZI CUP [Zanzibar]:

AMAAN STADIUM

(January 2-12):

Group ‘A’:

Simba[Tanzania Mainland]

Tusker[Kenya]

Jamhuri[Zanzibar/Pemba]

Bandari[Zanzibar]

Group ‘B’:

Azam[Tanzania Mainland]

Mtibwa Sugar[Tanzania Mainland]

Coastal Union[Tanzania Mainland]

Miembeni[Zanzibar]

FIXTURES:

Wednesday, January 2:

4.00pm:Tusker v Bandari

8.00pm:Jamhuri v Simba

Thursday, Jan 3:

4.00pm:Mtibwa Sugar v Miembeni

8.00pm:Azam v Coastal Union

Friday, Jan 4:

4.00pm:Jamhuri v Bandari

8.00pm:Simba v Tusker

Saturday, Jan 5:

4.00pm:Mtibwa Sugar v Coastal Union

8.00pm:Miembeni v Azam

Sunday, Jan 6:

4.00pm:Tusker v Jamhuri

8.00pm:Simba v Bandari

Monday, Jan 7:

4.00pm:Miembeni v Coastal Union

8.00pm:Azam v Mtibwa Sugar

Tue, Jan 8:

REST DAY

Wed, Jan 9:

8.00pm:SEMI-FINAL I

Thur, Jan 10:

8.00pm:SEMI-FINAL II

Fri, Jan 11:

REST DAY

Sat, Jan 12:

8.00pm:FINAL