Fainali za tano za Uhai Cup zitapigwa leo kwenye uwanja wa karume ambapo zitaikutanisha Azam Academy ambayo itakuwa ikicheza fainali yake ya nne (kati ya tano) na Coastal Union ya Tanga.
Azam Academy inayoundwa na wachezaji wengi wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao wengi wao wanachezea timu ya Taifa ya Serengeti Boys itajiaribu kulitwaa kombe ambalo msimu uliopita ililipoteza kwa Simba SC katika hatua ya penati baada mchezo kuisha dakika 90 kwa matokeo ya sare ya 0-0

Pamoja na fainali hizi kuingia mwaka wa tano lakini bado inaonekana wadau hawajaelewa dhana ya mashindano haya kwani tumeshuhudia timu nyingi zikileta vijeba tena baadhi ya wachezaji hao vijeba ni wale ambao walishachezea baadhi ya timu Kama Azam Academy na kuachwa baada ya kuvuka umri.
Tatizo hili linapoteza maana ya mashindano na linapaswa kukemewa kwa nguvu zote
Tunaitakia kila la heri Azam Academy iweze kushinda kikombe hiki na kuungana na kaka zao walioshinda ubingwa wa Congo Charity Cup hapo jana.