Wachezaji watatu wa Azam FC golikipa Aishi Salum Manula (Azam Academy), beki Samih Haji Nuhu na Khamis Mcha Viali wameitwa kwa mara ya kwanza kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayojiandaa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Zambia.

Kikosi hicho kimetangazwa leo na kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen na kitaanza kambi ya maandalizi kesho kikiwa na wachezaji 24 wa ndani na wanaocheza nje ya nchi.

Katika timu hiyo Azam FC inajumla ya wachezaji nane katika kikosi hicho kinachoundwa na makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20), mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Yanga).

 

Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC).

 

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi Kazimoto (Simba).

 

Stars itacheza dhidi ya mabingwa hao wa Afrika Desemba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.