Azam FC inatangaza msiba wa mchua misuli (Masseur) wake Khamis Mbembe uliotokea leo saa tano asubuhiKhamis Mbembe alikuwa mcheshi, muungwana na mchapakazi hodari ambaye anatuachia pengo kubwa sana klabuni.
Mbembe alipata maradhi

ya kupooza yaliyomsumbua kwa kipindi kirefu taratibu tangia June mwaka jana ambapo alipumzika kufanya kazi Azam FC Novemba mwaka jana ili kupata matibabu zaidi ambapo Klabu ya Azam FC na familia ya Mbembe kwa pamoja tulihangaika bila mafanikio. mwenyezi mungu alitoa na yeye ndiye aliyetwaaTunamuombea dua marehemu roho yake ipumzike mahala pema peponi. Amin

pichani Mbembe kushoto mwenye ndevu na koti jeusi akiwa na Katibu mkuu wa Azam FC Nassor Idrissa na kocha msaidizi Kally Ongala nchini Rwanda