Tuhuma zinazowakabili wachezaji wetu wanne zimekabidhiwa kwa chombo cha Serekali cha kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU, kisheria na kwa taratibu tuhuma zikikabidhiwa kwenye chombo husika kupisha uchunguzi, ni busara kwa watuhumu kukaa kimya ili kuwapa nafasi TAKUKURU wafanye kazi yao kwa uweledi. Azam FC inawaomba wapenzi na mashabiki wake kuvuta subira wakati wa kipindi hiki kigumu wakisubiri ripoti ya uchunguzi toka TAKUKURU.

Imetolewa na ofisi ya utawala
Azam FC