Zikiwa imebakia siku chache kabla ya mumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) Timu ya Azam FC imerejea katika nafasi ya pili baada ya kuifunga JKT Oljoro 1-0 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Ddar es Salaam.

Ushindi huo imefikisha Azam FC katikia nafasi hiyo ikiwa na jumla ya pointi 24, chini ya Yanga yenye pointi 26 na juu ya Simba yenye pointi 23, kila timu ikibakiza mchezo mmoja kumaliza mzunguko huu wa kwanza wa msimu wa 2012/13.

Azam FC katika mchezo huo ilikuwa ya kwanza kupata goli mapema dakika ya 3 kipindi cha kwanza kupitia kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Tchetche Kipre, penati hiyo ilimriwa na mwamuzi Livingstone Lwiza baada ya beki wa Oljoro Yasin Juma kunawa mpira katika eneo la hatari.

Goli hilo la Kipre Tchetche limeongeza idadi yake ya magoli ya kufunga na kufikia magoli saba tangu kuanza kwa ligi kuu, akiwa amecheza mechi 12.

Katika mechi hiyo iliyokuwa imejaa kila aina ya ushindani timu zote zilifanya mashambulizi lakini hazikuweza kubadilisha matokeo hayo.

Kipindi cha kwanza Oljoro walijitahidi kusawazisha bao hilo kwa kufanya mabadiliko ya kwanza katika dakika ya 15 alitoka mchezaji Meshack Nyambele akaingia Edmond Kashamile mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo lakini hayakubadilisha matokeo hayo na timu zikaenda mapumziko Azam FC ikiwambele kwa 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama cha kwanza, timu zikitengeneza nafasi lakini umaliziaji ukiziangusha timu zote, dk 56 John Bocco alifanya kosa kama la kipindi cha kwanza dk 34, kushindwa kumalizia krosi ya Tchetche na mpira kutoka nje.

Dk 87 mchezaji wa Azam FC, Himid Mao alitolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi huyo Lwiza kutoka kagera baada ya kumtendea madhambi mchezaji wa JKT Oljoro Amri Omary na kuisababishia timu yake kucheza pungufu kwa dakika 3 kabla ya mpira kumalizika.

Azam FC ilifanya mabadiliko walitoka Tchetche Kipre dk 68 akaingia Gaudence Mwaikimba na dakika ya 90  John Bocco alipumzika na nafasi yake kuchukuliwa na Samih Haji Nuhu mabadiliko hayo hayakubadilisha matokea na mpira kumalizika Azam FC ikipata ushindi wa 1-0 dhidi Oljoro ya mkoani Arusha.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Kocha wa Azam FC Stewart Hall alisema matokeo hayo muhimu kwa timu yake na kusikitishwa na nafasi za wazi alizokosa Bocco lakini ameridhishwa na kiwango chake na ushindi huo.

Stewart amesema muda huu mchache ulibakia ataendelea kukifua kikosi hicho ili kumalizia mechi ya mwisho dhidi ya Mgambo JKT siku ya Jumamosi.

Azam FC itaelekea mkoani Tanga, tayari kumalizia mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Mgambo JKT, utakaochezwa Jumamosi Nov 10 kwenye Uwanja wa Mkwakwani  mkoani humo.