Mabao mawili ya Dedier Kavumbangu na Khamis Kiiza jana yalipeperusha tena ndoto za Azam FC za kukaa kileleni kwa mara ya nne msimu huu.

Mara ya kwanza ilikuwa ni katika mechi dhidi ya Tanzani Prisons ambapo endapo Azam FC ingeshinda basi ingekwea hadi kileleni

Mara ya pili ilikuwa ni katika sare dhidi ya Ruvu Shooting Stars na baadaye ilipopoteza dhidi ya Simba kwa kufungwa 3-1.

Azam FC inabaki na pointi 21 na michezo miwili mkononi huku yanga ikitinga kileleni kwa mara ya kwanza kwa kufikisha pointi 26

Ligi hiyo itaendelea tena jumatano hii ambapo Azam FC itakwaana na JKT Oljoro Chamazi Dar es Salaam