Yamebaki masaa tuu kabla ya miamba miwili ya soka la Tanzania Yanga SC  (timu ya wananchi) na Azam FC kushuka kwenye uwanja wa Taifa jijina Dar es Salaam.

Picha juu ni kwa hisani ya Tovuti maarufu ya soka nchini ya Galacha (www.kandanda.co.tz)

Hii ni mechi ya kisasi, kwa kuwa Yanga watajaribu kulipa kipigo kichungu cha 3-1 kwenye ligi kuu huku Azam FC nao wakijaribu kulipa kipigo cha 2-0 kwenye CECAFA Kagame Cup.

Kuwa kutilia maanani uzito wa mechi ya leo, benchi la ufundi la Yanga lilitua Chamazi kujaribu kuifanyia ushushushu Azam FC huku wakiweka kambi Bagamayo utadhani wanajiandaa kukwaana na mahasimu wao wa jadi Simba SC.

Azam FC ambayo imeongezewa makali baada ya kumrejesha kocha wake anayeijulia sana Yanga Stewart Hall nayo imekuwa kambini Chamazi ikijiandaa na mtanange huo.

Vikosi vyote viwili havina majeruhi baada ya wachezaji wa Yanga Said Bahanuzi na Kevin Yondani kurejea kama ilivyo kwa Azam FC ambapo beki wake wa kushoto Waziri Salum amerejea kikosini kama ilivyo kwa John Bocco.

Akizungumza na Mtandao wa Azam FC, mshambuliaji Kipre Tchetche ambaye ndiye anayeongoza kufunga magoli msimu huu alisema wapo katika hali nzuri na inshallah kwa rehma za Mwenyezi Mungu Tutashinda.

Mechi hii itatangazwa moja kwa moja na Kiss FM