Azam leo inashuka kwenye uwanja wa Taifa kukwaana na Simba SC ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania (Vodacom Premier League)

Azam FC ambao jumatano iliyopita walitoka sare na JKT Ruvu Shooting leo watajaribu kushinda ili kujiweka kwenye usukani wa ligi kuu

Azam FC wataingia uwanjani wakitokea Chamazi ambako wameweka kambi kwa ajili ya mchezo huo huku Simba wakiingia uwanjani wakiwa wanatokea visiwani Zanzibar.

Wachezaji wote wa Azam FC isipokuwa Ibrahim Rajab Jeba ambaye ana majeruhi wapo katika afya na hali nzuri kwa ajili ya mchezo huo