Azam FC leo inajitupa kwenye dimba lake la Chamazi kukwaana na moja ya timu bora kabisa VLP ya Ruvu Shooting Stars.

Mchezo wa leo ni muhimu sana kwa Azam FC kwani utaihakikishia uongozi wa ligi kuu huku ikiwa na mechi moja mkononi.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Boris Bunjak amesema amekiandaa vema kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo na anatarajia matokeo mazuri.

Kiungo Abdulhalim Humud ambaye aliumia kwenye mazoezi na kukosa mchezo uliopita anatarajia kurejea dimbani leo kusaidiana na wenzake.

Webmaster anaiombea dua Azam FC, “Mungu Ibariki Azam FC”