Kesho katika dimba la Sokoine jijini Mbeya Azam FC itajaribu kushinda mchezo wa sita kati ya saba ya awali kwenye ligi kuu mbele ya Banyambala Tanzania Prisons

Azam ambayo inaungana na Simba SC kuwa timu pekee ambazo hazijapoteza mechi hadi hivi sasa ipo jijini hapa tangu juzi jumapili na leo ilifanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Sokoine ili kuuzoea.

Kocha mkuu wa Azam FC Boris Bunjak amesema kuwa amejipanga kuhakikisha kuwa timu inapata matokeo mazuri katika mechi ya kesho

Wachezaji wote waliosafiri na timu wapo katika hali nzuri isipokuwa Zahoro Pazi ambaye ana maradhi ya tumbo.

Endapo Azam FC itashinda mechi ya kesho basi itafikisha pointi 19, pointi tano tuu pungufu ya idadi ya pointi tulizojikusanyia msimu uliopita.