Azam FC kesho itashuka kwenye uwanja wa Jamhuri kujaribu kushinda mechi ya nne mfululizo na kuendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo hata mmoja pale itakapokwaana na Polisi Moro

Kocha Boris Bunjak amepania kushinda mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja mbovu wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kikosi cha Azam FC kiliwasili mjini Morogoro jana jioni na leo jioni walifanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Jamhuri.

Kikosi kinachotarajiwa kuanza kesho ni

GKMwadini Ally

DF- Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Moradi & Aggrey Morris

MD- Abdulhalim Humud, Jabir Aziz, Abubakar Salum & Himid Mao

ST- John Bocco, Kipre Tchetche