Licha ya kushika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi mbili tuu baada ya kufungwa mechi mbili na kutoka sare mechi mbili. Timu ya Polisi Moro ni moja ya timu zenye ukuta mgumu zaidi VPL ikiungana na JKT Oljoro, Simba  na Azam FC ambazo kwa pamoja zimeruhusu magoli mawili tuu kutinga kwenye nyavu zao.

Azam FC ndiyo timu pekee ambayo imeruhusu magoli kuingia kwenye mechi moja tuu baada ya kukubali kutoka sare 2-2 na Toto Afrika jijini Mwanza huku ikiwa imeondoka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye mechi tatu za ligi kuu.

Hadi kufikia raundi ya nne, Simba SC ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza pointi hata moja baada ya kucheza michezo minne na kushinda yote.

Polisi Moro imejiwekea rekodi nyingine kwenye VPL raundi ya nne baada ya kuwa timu pekee iliyocheza mechi nne bila kufunga goli hata moja.

Hadi kufikia raundi ya nne ya ligi kuu ya Vodacomkuna vilabu vinne tu ambavyo havijaruhusu kupoteza mchezo hata mmoja hadi sasa, vilabu hivyo ni  Toto Africa, JKT Oljoro, Coastal Union, Simba SC na Azam FC.

Klabu cha JKT Ruvu Stars ndicho kilichoruhusu magoli mengi zaidi ya kufungwa kikiwa kimefungwa magoli 10 hadi sasa kikifuatiwa na nduvu zao wa Ruvu Shooting Stars walioruhusu magoli nane kama ilivyo kwa wapiganaji wa African Lyon.

Kwa upande wa magoli ya kufunga klabu ya Simba SC ndiyo inayoongoza ikiwa na magoli tisa na kufuatiwa na Azam FC yenye magoli saba huku vilabu vya Ruvu Shooting Stars na Mtibwa Sugar vikiwa vimetikisa nyavu mara sita kila kimoja.

Wachezaji Kipre Tchetche wa Azam FC na Husein Javu wa Mtibwa ndiyo wanaoongoza kufunga magoli kwenye ligi kuu wakiwa na magoli matatu kila mmoja hadi hivi sasa.