Azam FC leo inajitupa kwenye uwanja wa Taifa kukwaana na timu ngumu ya  JKT Ruvu katika raundi ya nne ya ligi kuu ya Vodacom.

Mchezo wa leo ambao utaoneshwa na kituo cha televisheni cha Super Sports utaanza saa moja jioni.

Azam FC yenye pointi saba na inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu itapenda kushinda ili kurejea kileleni mwa ligi kuu.

Katika mchezo wa leo Azam FC itaendelea kumkosa Abdulhalim Humud ambaye alichanika nyama za paja lakini itafurahia kurejea kwa Salum Abubakar Sureboy ambaye amepona kutoka majeruhi.

Mshambuliaji John Bocco atajaribu  kuanza kufunga baada kucheza michezo mitatu iliyopita bila kufunga kinyume na kawaida yake.

Kikosi cha Azam FC kinachonolewa na kocha Boris Bunjak kinatarajiwa kuwakilishwa na wachezaji wafuatao

GK – Mwadini Ally

RB – Erasto Nyoni

LB – Haji Nuhu

CB – Said Moradi & Aggrey Morris