Azam FC leo imepaa hadi kwenye usukani wa ligi kuu baada ya kuifunga Mtibwa Sugar 1-0 na kufikisha pointi saba (7) goli limefungwa na Kipre Tchetche

 

Ushindi wa leo umevunja mwiko wa kupata matokeo mabaya dhidi ya Mtibwa jijini Dar es Salaam ambapo katika mechi nne za ligi ambazo Azam FC imecheza na mtibwa jijini Dar es Salaam taingia ipande daraja kabla ya mchezo wa leo. Azam FC ilifungwa michezo miwili na kutoka sare michezo miwili.

 

Msimu uliopita katika michezo mitatu (Mtibwa Dar es Salam, Toto na Kagera kule kanda ya ziwa) Azam FC ilivuna pointi mbili pekee tofauti na msimu huu ambapo tumeweza kuvuna pointi saba.

 

Katika mchezo wa leo, shujaa alikuwa ni kinda Himid Mao ambaye alicheza kuwa kujituma na kuharibu mipango yote ya Mtibwa. Kwa jinsi alivyoshirikiana na Jabir Aziz, waliwafanya Mtibwa kushindwa kuelewana na kuwafanya wapoteana kabisa.

 

Kiungo mwingine Ibrahim Mwaipopo na Abdi Kassim walitulia na kucheza kwa umakini huku pasi zao na mashuti golini mwa Mtibwa yakiwapa presha muda wote.

 

Azam FC itacheza mchezo wake wa tatu siku ya Ijumaa usiku dhidi ya JKT Ruvu mchezo ambao utaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Supersport

 

Azam FC; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Samih Nuhu, Said Moradi, Aggrey Morris, Himid Mao/Hamis Mcha Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim/Kipre Bolou John  Bocco na Kipre Tchetche