Mashabiki wa Azam FC kesho watakuwa na nafasi ya kuiona timu yao ambayo itakuwa imerejea toka ziara ya kanda ya ziwa pale itakaposhuka kwenye uwanja wa nyumbani kukwaana na Mtibwa Sugar

Katika msimu uliopita Mtibwa Sugar iliifunga Azam FC kwa maana hiyo Azam FC itataka kurudisha machungu ya kufungwa na Mtibwa msimu uliopita

timu zote zinajivunia kuwa na wachezaji wenye viwango vizuri na ambao wameshawahi kuchezea timu zote

Wakati Azam FC ina Abdi Kassim, Deogratius Munishi, Ibrahim Mwaipopo na Abdulhalim Humud ambao walianzia kucheza soka kwenye mashamba ya miwa. Mtibwa nayo ina Malika Ndeule, Salvatory Ntebe, Shaaban Kisiga na Jamal Simba Mnyate ambao wamewahi kuichezea Azam FC

Ligi ya msimu huu imekuwa na msisimko mkubwa na hamasa kubwa na inaonekana watanzania wengi sasa wanaifuatilia sana.