Ndugu wapenzi na mashabiki wa Azam FC, tunapenda kuwaomba radhi kutokana na kuchelewa kutoka kwa jezi zetu mpya za msimu wa 2012/13. Hii inatokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa klabu ya Azam FC

Kama mnavyojua klabu yetu inadhaminiwa na SSB ambao pia ni wamiliki wa klabu. SSB iliamua kuwa Jezi za msimu wa 2012/13 zitoke na nembo (jina) la bidhaa yetu mpya inayoitwa ‘Azam Energy Drink’ lakini kwa bahati mbaya hadi sasa SSB bado haijazindua kinywaji hiki.

Kutokana na kasoro hii, tumeona ni bora tukaendelea kutumia Jezi zenye nembo ya Azam Cola ili kuwaepusha wateja na usumbufu wa kuulizia kinywaji hiki kipya ambacho bado hakijaingia sokoni. Jezi mpya za Azam Energy Drink ambazo tayari zimefika zitaanza kutumika na klabu baada ya kuingizwa sokoni kwa kinywaji hiki kipya.

Lakini tunaomba tuwape habari ya kufurahisha, ambayo ni kwamba jezi zetu za Azam Cola pamoja na bidhaa nyingine kama kofia, Skafu na Tshirt za Azam FC kuanzia wikiendi ijayo zitaanza kupatikana kwenye maduka mbali mbali ya nguo na vifaa vya michezo kama UHL Sports la Kassim Dewji, Street Soul, ML8T na Zizzou Fashion kwa gharama za shilingi 20,000 tuu.

Kwa wale wote wenye nia ya kuuza bidhaa hizi popote nchini tafadhari wasiliana na klabu ya Azam FC kwa email email (info@azamfc.co.tz) ili kupata maelekezo ya jinsi ya kuzipata

Imetolewa na uongozi