Mshambuliaji John Bocco wa Azam FC ameifungia timu yake magoli mawili ya ushindi ya Coastal Union katika mchezo wa karafiki uliochezwa leo kwenye uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo huo Azam FC imepata ushindi wa 2-0 dhidi ya timu hiyo matokeo ambayo yameifanya Azam FC kuweka rekodi ya kushinda michezo mitatu mfululizo ya kirafiki.

Bocco alianza kuonyesha uwezo wake mapema katika mchezo na kuandika goli la kwanza dk 15.

Azam FC inayojiandaa kucheza na Simba katika mchezo wa ngao ya Jamii, imeonyesha kubadilika na kucheza mchezo wa kasi na kuimarisha safu ya ulinzi.

Coastal Union katika kipindi cha kwanza hawakuonyesha makali yao na kuwafanya Azam FC kutumia nafasi hiyo kuandika bao la pili lililowekwa wavuni na Bocco aliepiga shuti liligushwa na kipa Jackson Chove na kuingia wavuni katika dk 44 ya mchezo.

Bao hilo lilizipeleka timu mapumziko Azam FC wakiongoza 2-0 dhidi ya Coastal Union.

Kipindi cha pili kilianza Coastal wakifanya mabadiliko walitoka Othman Omary, Binslum na Papy Mbaligwe nafas zao zikachukuliwa na Razak Khalfan, Juma Jabu na Nsa Job mabadiliko haya yaliimarisha timu hiyo na kuongeza mashambulizi lakini hayakubadili matokeo hayo.

Wachezaji wa Azam FC muda wote walikua imara, walifanya mabadiliko alitoka Jabiri Aziz aliyehimili sehem ya kiungo mkabaji akaingia Himid Mao, akatoka Kipre Tchetche na Bocco aliefunga magoli yote wakaingia Zahor Pazi na Gaudence Mwaikimba kabla ya kuingia Samir Haji Nuhu aliyeingia kuchukua nafasi ya Michael Bolou.

Mabeki Ibrahim Shikanda, Agrey Moris, Erasto Nyoni na Said Morad walisimama vyema katika nafasi zao kwa kuzuia mashambulizi yote ya Coastal Union.

Abdi Kasim alicheza dakika zote 90 amerejea katika kiwango chake na kumudu vyema sehem ya kiungo akiwa na Michael Kipre na Jabir Aziz, huku Bocco na Tchetche Kipre waking'aa upande wa ushambuliaji kwa kuingia kwenye eneo la Coastal mara kwa mara.

Katika mchezo ambao langoni kwa Azam FC alikuepo kipa Deogratius Munishi, mchezaji Abdulhalim Humud wa timu hiyo alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonywa kwa kadi mbili za njano katika dk 23 kipindi cha kwanza na kuifanya Azam FC kucheza pungufu.

Azam FC itaendelea na maandalizi ya ligi kuu na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Sept 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mazoezi yote yatafanyika kwenye uwanja wa Azam Complex.