Baada ya wiki iliyopita kuifunga Transit Camp 8-0, Jana Azam FC iliifunga Tanzania Prisons 1-0 goli likifungwa na Ibrahim Mwaipopo katika dakika ya 34

Mshabuliaji John Bocco ambaye alianza na Papi (Mkongo aliye kwenye majaribio na baadaye kuwapisha Kipre Tchetche na Gaudence Mwaikimba wote walicheza vizuri sana katika mechi hiyo licha ya kushindwa kufunga kutokana na kukusa bahati

Katika mchezo wa Jana Prisons ilifanya shambulizi moja tuu, lakini Azam FC muda wote walikuwa kwenye lango la Prisons

Viungo Abdi Kassim, Jabir Aziz, Abdulhalim Humud na Ibrahim Mwaipopo walitawala sehemu ya kiungo na kuwachanganya maadui. Kila mmoja wao alipata nafasi ya kupiga mashuti golini mwa adui ingawa mipira yao ilipaa au kuokolewa na kipa wa Prisons

Katika Mchezo wa Jana Abdulhalim Humud ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo

Azam FC ilikwakilishwa na Deogratius Munishi, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris, Said Moradi, Erasto Nyoni/Waziri Salum, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz/Himid Mao Abdi Kassim, Ibrahim Mwaipopo/Kipre Bolou, John Bocco/Kipre Tchetche, Papi/Mwaikimba