SIMBA itakutana tena na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Super8 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar esa Salaam baada ya jana kuifunga Zimamoto mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. huku Azam FC ikiifunga Polisi Moro 2-1. Magoli ya Azam FC yalifungwa na Abdi Kassim na Said Moradi

Timu hizo zitapambana tena, siyo zaidi ya wiki tatu tangu zilipokutana kwenye uwanja huohuo katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Kagame na Simba kulala 3-1.

Nusu fainali nyingine ya michuano hiyo itakuwa kati ya Jamhuri ya Pemba dhidi ya Mtibwa ya Turiani, ambayo pia itachezwa Uwanja wa Taifa.

Shujaa wa mabao ya Simba kwenye mchezo wa Moshi alikuwa mshambuliaji, Edward Christopher aliyekwamisha wavuni mabao yote mawili.

Kwenye Uwanja wa Chamazi, Jamhuri iliionyesha kazi timu ya Mtende kwa kuisigina mabao 4-0, ambapo mpaka mapumziko washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Mabao ya Jamhuri yalifungwa, Sadik Rajab katika dakika za 28 na 45, kabla ya Seleman Nuhu kufunga bao la tatu dakika ya 82, na la nne likifungwa na Seleman Ally dakika ya 90.
Habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
www.mwananchi.co.tz