Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa kuwa mkataba wake na kocha Stewart John Hall kutoka nchini uingereza ulisitishwa rasmi jana Tarehe 31/07/2012 kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Klabu ya Azam FC inajivunia mafanikio ya kocha Stewart Hall, na inampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika muda wote aliofanya kazi kama kocha mkuu na mkurugenzi wa ufundi.

Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame. Haya ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wote waliotangulia na ni mafaniko ya kihistoria katika klabu ya Azam FC.

Azam FC inamtakia kocha Stewart Hall kila la heri, na inatarajia kuwa ipo siku katika siku za usoni kocha Stewart atarudi tena kufanya kazi na Azam FC.

Stewart Hall anaacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake ambaye atatangazwa hapo baadaye lakini kizuri ni kuwa, mrithi wa Stewart Hall atakuwa ni mwalimu anayefuata mfumo ule ule wa uchezaji ulioachwa na Stewart Hall kwani hiyo ndiyo (Playing Philosophy ya Azam FC)

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Vivek Nagul na Kally Ongala

Imetolewa na Utawala

Azam FC