Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa milango iko wazi kwa klabu yoyote kumnunu mchezaji Mrisho Ngassa kwa gharama ya $ 50,0000.

Azam FC imefikia hatua hiyo baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na mapenzi na klabu hiyo na badala yake kuipenda klabu aliyotoka ya Yanga.

Hivyo uongozi wa klabu unapokea maombi kwa klabu yoyote inayomuhitaji mchezaji huyo.

Azam FC ilitoa nafasi ya upendeleo kwa klabu ya Yanga lakini hakuna ofa iliyoletwa kuhusu, klabu imepokea ofa kutoka Simba kumuhitaji mchezaji huyo.

Ngassa anauzwa siku chache baada ya kukubali kuvaa jezi ya Yanga na kuibusu logo ya timu hiyo, baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali kati ya Azam FC na AS Vita Club ya Congo DRC katika mashindano ya Kombe la Kagame yaliyomalizika Julai 28 mwaka huu.